Poleni najaribu kujivunia lugha la swahili
Nimekuwa mwenye mawazo nyingi sana. Nimekuwa nikiandamwa na zimwi la lugha, jinamizi ambalo limekataa kuniwacha kabisa. Swahili lugha ya kupendeza lugha ambayo najivunia kuongea kila saa na kila mahali. Lakini ikikuja kwa uandishi na kusoma na kitoroka kama ugonjwa, kwa nini?
Tuende pamoja niwaeleze. Kutoka shule ya msingi darasa la kwanza hadi shule ya upili kidato cha nne, yote jumla ya miaka kumi na mbili, Swahili limekuwa somo kama Kifaransa ama lugha nyingine la kigeni. Chakushangaza ndio lugha tunaongea na wanafunzi wenzetu, ndio lugha tunakizungumza kila mahali. Lakini ikifika kwa masomo kinageuzwa kuwa kitu kigeni kabisa.
Nilikuwa najipata na anguka swahili ukulinganisha na masomo zingine, kwa masomo zangu za miaka kumi na mbili. Katika mtihani wangu wa mwisho wa kidato cha nne swahili ndio ilikuwa somo langu lenye makisi ya chini kabisa C+
. Kwangu kusoma lugha ilikuwa kama kukweya mlima nikilinganisha na somo kama ya sayansi. Ni huzuni mtupu nikiwaelezea kwamba hadi sasa ikikuja ni uandishi na pata ugumu kuandika kwa swahili ukilinganisha na kizungu.
Nikiongelesha wenzangu napata pia hao, masaibu ni yale yale. Na ninabaki nikijiuliza kweli bado najivunia lugha hii?
Wengi ambao wataona uandishi huu watalipuuzilia mbali sana kwa vile wanapata ugumu kusoma swahili sanifu. Sina ubaya wowote na lugha zingine nimelelewa nikiongea ‘Sheng’ hata sasa tukizungumza utapata hiyo ndio lugha nitatumia. Lakini swali ni, Je, lugha hii (Sheng) unafuata maudhui ama sheria za lugha ghani? Kama haina sheria wowote ule ya maanisha ni ngumu sana kulifundisha na kulitahini shuleni. Labda tunahitaji kulifanyia utafiti, na kuandika na kutia msingi fulani amabazo zitafanya liwe lugha kamilifu.
Najua maandishi yangu yana makosa na dosari si haba, na hapo ndipo shida zangu zaanzia. Sina ule uwezo wakuirekebisha kwa vile ata sijui vizuri ni wapi makosa hayo yamo. Matumizi yangu ya ngeli, misamiati na kadhalika ni mbovu kabisa. Naomba msahama kwa walimu wangu wa Swahili kama vile Mbwana. Oganga na Bi. Mbua, miaka kadha mlijaribu kunifundisha lugha lakini sikutia maanani. Lakini pia niko na ubishi na nyinyi kiasi, kwa nini tulipokuwa tunamaliza somo la swahili tukikutana inje la darasa, tunalazimika kuwaongelesha na kizungu. Mbona tulikuwa na siku imetengwa kwa wiki kuongea kizungu, lakini lugha la swahili halikuwa pia nayo siku. Ndio na elewa kwamba tulikuwa tuonaongea “Swahili” kila wakati lakini ukisikiza vizuri haikuwa sanifu hata kidogo.
Sasa nimemaliza shule. Natumia mitandao kila saa, kazi yangu na marafiki wangu wote nawapata mtandaoni na tunazungumza. Gumzo zinanoga kabisa, lakini lugha tunatumia ni mchanganyiko usio na asili yeyote. Tunazungumza na ile “Sheng” yetu kwenye mtandao. Tumekuwa sasa wazazi, watoto wetu wameanza kusoma lugha ya swahili. Niko na uchungu kwa vile siwezi wasadia kuwakosoa mahali ambapo wamekosa. Ata wenzangu mtandaoni hawanikosoi nikipeperusha ujumbe mtandaoni wenye makosa ya lugha. Lakini wacha niandike ujumbe kwa lugha ya kizungu tutapata maelfu ya wenzangu wakini kosoa. Nitajitetea kwa kusema Kizungu kilikuja na meli, kusema ukweli ata swahili enyewe siezi kulidandika kwa kujiamini[Neno hili imebidi nitafute usaidizi mtandaoni kwa vile nilikuwa naijua kwa kizungu kama “confidence”] aibu ilioje.
Na aibika sana kuweka kwa “CV” yangu kwamba nazungumza na kuandika swahili vizuri ilhali mimi mwenyewe najua hii yote si ukweli kamilifu. Wengi ambao wamejaribu kupata mashule za ulaya wanaambiwa watoe thibitisho ya kwamba wanakifahamu vizuri kiingereza. Inawabidii wamefanya mtihani wa “IELTS” na “GMAT”. Wangapi tungekuwa na mtihani kama huo wa swahili tungepita?
Kizazi kipya na ata kizazi cha sasa, wanauliza kila mara ata nikikuwa gwiji wa lugha ya swahili nitasaidika vipi na sitakuwa mtangazaji wa habari. Swali hili ni nyeti sana, sina jibu lakini nitajaribu.
Kama wanakenya lugha hili ni la kitaifa na ni lugha ambalo tunaeza jivunia kama hadhifa ya taifa na tamaduni yetu. Wengi wetu mimi nikiwa mmoja wao, hatuwezi zungumza lugha ya mama na tofauti yetu na mzungu amabaye hajui swahili ni hiyo tu lugha ya swahili. Basi ya maanisha kwangu lugha hili la swahili ndio tamaduni yangu, ndio kitu ambayo inanitafautisha na watu wengine wa ulimwengu.
Nikiangalia hifadhi yangu ya vitabu, asili mia moja ni kizungu. Nataka kujitia motisha kuanza kusoma vitabu vya swahili. Ata kama itabidii ni some tamdhilia za shule za msingi na za upili nitanunua na kuvisoma. Imekuwa sasa miaka nyingi tangu niandike ujumbe mrefu kama huu kwa kiswahili. Mara yangu ya mwisho ulikuwa mtihani wangu wa mwisho wa kidato cha nne, karatasi ya pili ya kiswahili nikitahiniwa.
Labda tunahitaji kuanza kujivunia tena lugha hii pasi na hivyo litazikwa kwenye kaburi la sahau.